Taarifa

Bank M Yasimika Mfumo wa Google App kukabilina na changamoto za kibiashara.

Hatimaye Bank M. imekua bank ya kwanza Tanzania kuhamia katika mfumo wa Google Apps katika kijipanga kibiashara,mfumo unaoweza kumuwezesha mteja kuunganishwa kwenye mawingu(Cloud) na kuendelea na kazi sehemu yoyote huku akiwa na uwezo wa kuangalia mafaili yake kwa kutumia kifaa chochote cha kitekinilojia kama simu ya mkononi(Smart phone) ama komputa pakato(laptop).

Kwa mijibu wa Google mfumo huo unatoa zaidi ya asilimia 99.9 makubaliano ya huduma kwa mteja (SLA) na pia unampa kila mtumiaji nafasi ya kuhifadhi taarifa katika stoo ya kufikirika kwenye mawingu ama cloud, huku ikiwa na uwezo mkubwa wa kudhibiti barua pepe zisizotarajiwa ama spams. pia inaruhusu muingiliano wa tekinolojia zingine kama za blackberry ama MS outlook na pia ni rahisi kuunganisha na kutumia.

Akiongea kuhusu matokea ya kusimikwa kwa mfumo huo mpya mkurugenzi mkuu msaidizi wa Bank M Jacquiline Woiso amesema “Wanafuraha kubwa kuhamia kwenye mfumo huo ambao wanamatumaini utaongeza tija na ufanisi katika utoaji wa huduma za Bank M kwa ubora uliotukuka.

Mkuu wa kitengo cha TEHAMA wa Bank M, Ndg. Vinesh Davda amesema uamuzi wa kuhamia katika mfumo wa Google Apps ni uamuzi sahihi katika kukabiliana na changamoto za kawaida za kutanuka kwa biashara katika zama hizi za utandawazi.

________________________________________________________________________________________________

Hatimae Nokia wajisalimisha kwa Microsoft 3/9/2013.

Kampuni ya Microsoft imeinunua kampuni inayotengeneza simu za mikononi aina ya NOKIA. Wachambuzi mbalimbali wa mambo ya tekinolojia wanadai kwamba hatua hii imefikiwa ili kuongeza mapato ya Microsoft na kumuwezesha kumudu ushindani wa makampuni mengine kama sumsung na Mac ambao mbali na kujishughulisha na utengenezaji  wa mifumo endeshi ya simu na kumputer zao pia wamekua wakijishughulisha na utengenezaji wa vifaa vyenyewe kwa maana ya Hardware.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Lenduli Technologies

%d bloggers like this: