Elimu

HATUA ZA KUCHUKUA BAADA YA KUFIKIRIA KUMILIKI BLOG

Siku hizi katika Afrika mashariki kwa ujumla na Tanzania kwa uchache kumekua na wimbi la watu mbalimbali wakianzisha blogs ama Majarida la kielektroniki kwa malengo ya kutoa hisia zao ama kuhabarisha jamii na baadhi wamejikuta wakirukia tu kuwa na blog ambazo kwa kweli si dhani kama zimekuwa zikiakisi malengo ya waasisi wa blog hizo hivyo leo nimeamua kuwashushia japo kwa ufupi tu, ili angalau mpate mwanga wa kitu gani kinatakiwa kufanyika.

1.Ili kuanzisha blog ama jarida la kielektroniki unatakiwa kuchagua kampuni mwenyeji wa blog ama jarida lako la kielectroniki, hivyo kabla ya kuchagua basi ni lazima kufanya utafiti ili uweze kujua ni kampuni ipi inaweza kukidhi matarajio yako.

2.Unatakiwa kuchagua programu mujarabu kwa ajili ya kuunda blog yako, hii ni kutokana na kuwa na utitiri wa program ambazo zingine ni ngumu sana kuziunda kwa jinsi ya malengo na  unavyotaka wewe.

3.Programu hizo na makampuni hayo mwenyeji yanapatikana kwa gharama, Na mara nyingi bei zake hua ni tofautitofauti kutokana na muundo wa malipo, nyingine huchaji kwa mwezi ama kwa bure kabisa kwa gharama ya kuyaacha matangazo yao kwenye blog yako.

4.Ni muhimu kujua kwa ufasaha malengo ya blog yako halafu kufanya utafiti wa kina wa makampuni mbalimbali uanayohisi yanaweza yakawa mwenyeji wa jarida lako la kielektroniki ama blog na kama makampuni haya yanaweza kuifanya blog yako ifikie malengo yake

5.Mwisho unaweza ukawasiliana na watafiti na wachambuzi  wa masuala ya Tehama kama LenduliTechnologies (hawa wamebobea katika tafiti na uchambuzi wa tekinolojia mbalimbali) ili waweze kukushauri uchague kampuni ipi kulingana na malengo yako.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Lenduli Technologies

%d bloggers like this: