All posts by lenduli

JE TUNATUMIAJE SIMU JANJA, PAMOJA NA MITANDAO YA KIJAMII?

Jinsi unavyoweza kuhatarisha maisha yako marafiki zako na jamaa zako kwa kutumia mitandao ya kijamii
Mitandao ya kijamii kama facebook, instagram, badoo nk ni mitandao amabayo imejipatia umaarufu mkubwa sana hasa katika nchi za dunia ya tatu kwa siku za hivi karibuni.Umaarufu wa mitandao hii umetokana na tabia ya asili ya umbea ya wakazi wanoishi kwenye dunia ya tatu na kujikuta wakipost vitu ambavyo vimekua vikiwaharibia maisha yao kwa kiasi kikubwa bila wao kufahamu na kupata madhara ya muda mrefu yanayoweza kupelekea matatizo ya kisaikolojia ama hata kifo. Sababu ya pili iliyofanya mitandao hii kuwa maarufu zaidi ni kushuka kwa bei ya simu janja (SMART PHONES) hivyo kupelekea upatikanaji wake kuwa rahisi zaidi na kupelekea watumiaji wengi kuweza kumiliki simu hizo na kujiunga kwenye mitandao hiyo ya kijamii bila kuwa na elimu sahihi juu ya malengo na madhumuni ya kuwepo kwake hivyo kujikuta wakipost vitu ambavyo sio tu vinawafunua wao binafsi bali pia jamaa zao na mataifa yao kwa ujumla na hivyo kupelekea mmomonyoko wa maadili Machafuko, Utekwaji, na udahalilishaji katika taifa. Kwa mfano ni jambo la kawaida siku za hivi karibuni kumkuta mtu amepiga picha ya utupu, ama nusu uchi ama kaburi kwenye hizi nchi za jumuia ya tatu na kuandika status kwenye mtandao wa kijamii guu la bia, kiuno nyigu ama ndo tunazika sasa, ama mtu anampongeza mke wake, mume wake ama motto wake anaekaa nae nyumba moja kwenye mtandao wa kijamii, ama mtu anamtukana jirani yake kwenye mtandao wa kijamii, ama mtu anakula chakula cha jioni halafu anaandika status inatokea sasa hivi (It is happening now) na mambo kadhaa ya kushangaza bila kujua kuwa hayo ni mambo yake binafsi na yalitakiwa kuendelea kuwa binafsi.
Mimi nadhani matumizi bora ya mitandao ya kijamii ni kama kutangaza biashara ama ujuzi wako ili uweze kufahamika na labda ikuletee tija.
Ushauri wangu ni kuwa jamii yetu pamoja na utamaduni wetu wakutopenda kufanya kazi na kujikita zaidi kwenye mambo ya umbea ni lazima tutambue kuwa unapoweka kitu kwenye mtandao inamaana umekiweka ili kila mtumiaji akione hata kama ni chako binafsi wazungu wanasema (Once online it is there to stay) ina maana mtoto wako ambaye hata bado hajazaliwa siku akikua hata kama wewe umefariki anaweza kuona vitu vya hovyo ulivyokua unaposti. Mimi nikiamua kuwa mwizi na kwakutumia taaluma yangu ya kuzifahamu tekinolojia mbalimbali za mawasiliano ninaweza kukuibia kutokana na information zako unazoziweka mtandaoni kwa kutumia ukandarasi wa kijamii ama (Social engineering), mtekaji anaweza kukuteka, Majasusi na watu wenye husda ni rahisi kuifanyie nchi yetu ujasusi kwa kutumia taarifa tunazopost kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia teknolojia ya (big data mining) na kizifanya nchi zetu zisiendelee kiuchumi kwa sababu ni rahisi kukusanya taarifa za uelewa wa watu wan chi fulani kwa kuanza kukusanya taarifa zao kwenye mitandao ya kijamii ka facebook, instagram, watsapp, badoo n.k
Pia ningependekeza serikali iongeze maradufu kodi za simu janja (smart phones) ili zisiwafikie watu wengi zaidi na kuleta matatizo kama hayo niliyoyataja hapo juu.

Advertisements

Why Windows 9 Is Likely to Be More Successful Than Windows 8

Microsoft (NASDAQ: MSFT  ) intends to release Windows 9 in April 2015, about one year from now, perhaps to appease the masses that have revolted against Windows 8. For all its failings, Windows 8 is perhaps the most maligned Windows OS in recent history. It has been labeled an unmitigated disaster both from an end-user viewpoint and from Microsoft’s perspective in terms of adoption rates.

But according to a recent NetMarketShare study, Windows 8 has a 6.38% market share, almost double the market share for Apple‘s (NASDAQ: AAPL  ) Mac OSX 10.9 with 3.48%, although the latter has only been around for just six months. Windows 7 has the lion’s share of the market with 47.31%.

Windows 8 adoption rate not as bad as feared
There is no denying that Microsoft bet the farm by developing an OS targeted at both touchscreen devices and the traditional desktop. The result? Windows 8 is not perfectly suited for either platform, and desktop users in particular find it needlessly difficult to use.

Microsoft recently released data that showed that it had sold over 200 million Windows 8 licenses. Windows 8 is now about 19 months old since its release in August 2012. By the time Windows 7 had been in the market that long, Microsoft had managed to sell 240 million licenses for the OS. But let’s not forget that PC sales have been steadily declining, with shipments falling a jaw-dropping 10.3% last year. Most Windows OS purchases are tied to new PC purchases.

During the period that Microsoft sold 240 million Windows 7 licenses, 350 PCs were shipped worldwide. That works out to about 68 licenses for every 100 PCs sold. In comparison, 314 million PCs were sold during the period that Microsoft sold 200 million Windows 8 licenses. That works out to 63 licenses for every 100 PCs sold. While that might not be on an equal footing with Windows 7, it’s much better than the 55 licenses per 100 PCs for Windows XP, or 37 PCs for every 100 PCs sold that Windows Vista recorded, in a similar time span.

Exit of Windows XP creates room for Windows 9
Microsoft plans to withdraw support for Windows XP in April this year. A study done by TechProearly this year showed that 37% of Windows XP users plan to continue using the OS even after Microsoft withdraws its support

The erosion of IT’s middle class

Makala hii nimeamua kuibandika kwa lugha yake kutokana  na umuhimu wake  hasa kwa wataalamu wa ICT, kwa hisani ya  DS mchambuzi nguli wa masuala ya ICT Tanzania.

If you are a mid-level IT staff member, you will need to improve your
skills to move into that top tier and preserve your place in an IT
organization. If you fail to make that transition, then you are likely
to suffer “brain drain” and you will move into that lower tier.

If you have spent a lot of time in the IT industry and you are just now
reaching that middle-tier skill set, your career is at a crossroads. You
can choose to stay where you are, but in doing so you risk being made obsolete by a robot or Java/Python script. If this scares you, then you
should invest in your professional development, learn to be
cross-functional, and try to learn how to control the software components that will make you more efficient at your job.

However, if you are at the lower tiers of the IT food chain, you can rest assured that your “smart- hands” will continue to be needed. As Judge Smails in the movie Caddyshack said so eloquently, “Well, the world needs ditch diggers too.”

These developments are driven by a number of things. Among them: the rising cost of “down-time” as organisations become more and more reliant on IT; the rising cost of real-estate and energy for power+cooling as the hardware assets are increased; the fixed overhead costs of IT resources (people+kit) that cannot by elastically adjusted according to the business environment; the very tangible demand for mobile-access to systems by clients and staff alike; the fact that factories are inevitably evolving their products towards reducing their own costs of production and management by taking advantage themselves of outsourcing and Cloud.

There are additional reasons, that list can be much longer, but those
that I have mentioned are among the main factors that are being
considered by CEOs and their Finance departments when seeking greater value-for-money out of the investments they are being forced to make into IT. And the impact is that of reducing the “middle-class”, as described.

I must admit that prior to my joining IBM, this trend was much less
noticeable to me. But with the exposure I am now getting to the inner workings of our labs, factories, customer priorities, all around the globe, I can say that denial or resistance is futile especially now that “Cognitive Computing” has become a reality.

Many of you may not believe this but back in 1986 or so, I was
pooh-pooh’d big time for saying that one computer per organisation was insufficient, instead the future would be of one on every desk and all inter-connected to share data. Then the same happened in 1994 for saying that fax and telex would soon be rendered obsolete due to the Internet.At present we’re on the verge of seeing IT, after helping to better manage or automate our manual job-flows, is increasingly helping to better manage or automate our IT job-flows too…

So definitely, people in IT-based jobs need to keep on evolving their
skills to stay ahead of the technology and not become the victims of its evolution. Reading the article shared by Dharmin is a good start. And exploring the resources offered by the authoritative and diverse http://www.coursera.org http://www.coursera.org could be a useful next step…

With regards,
DS.

Katika kupambana na washindani wa Biashara Microsoft ameamua kuchanganya program endeshi za Nokia na mfanano mpya wa program endeshi za Android, familia ya X

Mwezi huu wa pili NOKIA wamethibitisha kuwa utakua ni mwezi wa mafanikia katika soko la Simu kutokana na uamuzi wao wa kuleta Nokia familia ya X sokoni zinazotumia program endeshi za Android.

Msemaji wa NOKIA alisema kuwa familia ya  X, X+ na XL zitakuwa simu za viganjani zenye uwezo mkubwa (smartphones),  zitakua zinauzwa kiasi cha dola za kimarekani 123, 136 na 150, kila moja.

Ameendelea kusema kuwa kama ilivyo kwa simu za bei nafuu za NOKIA Asha, Nokia familia ya X  zitakuja na rangi angavu kwani wameazima baadhi ya tabia za NOKIA Asha.

Aliendelea kusema kuwa lakini kama ailivyokua kwa NOKIA ASHA, nokia familia ya X haitauzwa kwenye soko la Marekani. Kwani mstari wa biashara umekusudiwa kwa nchi za Ulaya,Asia,India,Amerika ya kusini, Mashariki ya Kati na Afrika.

Hata hivyo aliweka bayana kuwa simu hizo za familia ya X  zitakua ghali kidogo kuliko ASHA ambazo zilikua zinauzwa si chini ya dola 73 za kimarekani

– kwa taarifa Zaidi tembelea: http://www.linuxinsider.com/story/80027.html#sthash.YhoPpfwH.dpuf

Imetundikwa na Martin K; lenduli@yahoo.com, mchambuzi sugu wa Mifumo ya tehama.

Tovuti ya Certified Ethical Hacker (CEH) yavamiwa.

Mvamizi wa mitandao aliyejitambulisha kwa jina la “EUGEN Belford” ameuvamia mtandao wa EC-Council Website,mtandao unaomilikiwa na wavamizi waadilifu wa Mitandao (ETHICAL HACKERS).

Ujumbe uliokuwa umetundikwa katika tovuti hiyo ulisomeka “Tovuti hii inamilikiwa na wavamizi wa mitandao wasio waadilifu”

Pia ujumbe mwingine ulisomeka “Edward Snowden” anahudhuria mafunzo ya uvamizi wa mitandao wa kiadilifu inchini India”

Msemaji wa shirika la CRPF kwa kiswahili (Walinzi wa usiri na uvamizi wa mitandao) alisema “wamefanya shambulizi la kuteka DNS na kuivamia tovuti hiyo na kuna uwezekano mkubwa pia kuwa wamefanikiwa kuona barua pepe za taasisi hiyo”.

Msemaji mwingine wa CEH amesema kuwa japokua mitaala, mafunzo na vyeti  vinayotolewa na CEH ni bora lakini mara nyi wamekua hawana uwezo wa kukabilina na wavamizi wa mitandao.

Hata hivyo baada ya habari hizi kuvuja kwenye mitandao mbalimbali wavamizi walifanya marekebisho ya ujumbe na kuongeza maneno yafuatayo:-

“kazi nzuri kuendelea kutumia nuila yako/neno la siri(PASSWORD) morans jack6783@, inamilikiwa na wavamizi wa mitandao wasio waaminifu kiungo chetu ni http://attrin.org/erratu/charlatan/ec-council/ EUGEN BELFORD “Tafadhali inawezekana wengi wenu mmechanganyikiwa nimeketi nyumba ya maelfu ya pass za kusafiria zinazomilikiwa na LAW ENFORCEMENT & MILITARY OFFICIALS”.

Imetundikwa na Martin K . kwa msaada wa E-Hacking news.

WASIMAMIZI WA TOVOTI WAMEJIPANGAJE NA UVAMIZI WA MAHARAMIA WA MITANDAO?

Hii ni kutokana na kuvamiwa kwa tovoti mbalimbali za serikali ya Venezuela na kundi la maharamia wanaojiita anonymous Venezuela

Miongoni mwa tovoti zilizovamiwa na kundi hilo la maharamia ni zile zinazomilikiwa na Jeshi la Venezuela kama tovoti ya (hidropaez.gob.ve), tovoti ya chuo cha kiufundi cha kijeshi (atmb.mil.ve),taasisi ya kijeshi inayojishughulisha na masuala ya kiitelijensia (dgim.mil.ve), Tovoti ya polisi ya Aragua (policiamunicipalvargas.gob.ve), Pia kundi hilo lilifanikiwa kuivamia tovoti ya chuo kikuu cha Falcon (udefa.edu.ve), Kwenye tovoti hizo walibandika ujumbe uliosomeka “Sisi si wavunja sharia(Criminals) bali si raia tunaopaza sauti ya kutoridhishwa na hii kitu inayoitwa serikali, na muda mchache ujao kuna mengi zaidi yatafuata”
SWALI: Je sisi kama  sisi kam nchi zilizopo kwenye jumuia ya Afrika Mashariki  tumejipangaje hasa kwenye Nyanja ya Cyber security kwa upande wa mitandao ya taasisi za serikali na binafsi, je tunao watu kwenye taasisi zetu wanaoweza kutusaidia? kama hakuna tunafanya nini basi?
Imeandikwa na Martin K. mtafiti wa masuala ya usalama wa mitandao,na mchambuzi sugu wa mifumo ya komputa.Unaweza ukawasiliana nae kwa barua pepe lenduli@yahoo.com ama kwa simu namba 0717 063292 kwa ushauri kuhusu tekinolojia ya habari na mawasiliano.

Bill Gates, Ctrl-Alt-Delete; Ilikua ni kosa

 

Ni kitu ambacho angalau ni lazima kukifanya kila siku kabla ya kuanza kazi ama kuanza kurambaza kwenye tovuti mbalimbali tukiwa majumbani mwetu, tunalazimika kubonyeza vitufe vya Ctr-Alt-delete kwenye keyboard zetu kujitambulisha kwenye komputa zetu.

David Roubenstain mwenyekitu mtendaji katika chuo kikuu cha havadi katika mahijiano maalumu aliyoyafanya na nguli wa program tumishi na endeshi za macrosoft  Bill Gates mwishoni mwa wiki katika chuo kikuu za havadi, Alilimuualiza mtaalamu nguli wa program za Microsoft ni kwa nini ilikua ni lazima kutumia vitufe vitatu badala ya kimoja. 

lilikua ni kosa kubwa kutumia vidole vitatu badala ya kimoja kujitambulisha kwenye komputa kabla ya kuanza kazi, tungeweza kuwa na kitufe kimoja lakini aliyetengeneza keyboard za IBM hakutaka kutupa nafasi ya kuwa na kitufe chetu kimoja, lilikua ni kosa, Microsoft imefanya vitu kwa upeo wa hali ya juu na pia tumejaribu vitu vingi kwenye program lakini sio kwa upande wa hardware”. 

Ukarabati wa Bishara (Business Reengineering)

Watu wengi na hasa wafanyabiashara wadogo na wakati wamekua wakijiuliza Ukarabati wa biashara ni nini (Business Reengineering)?, Hivyo basi leo kwa makusudi  nimeamua kuwaelimisha kuwa ni kitu gani? na ni kwa nini ni mumuhimu kukarabati biashara yako.

Ni lazima tutambue kuwa uendeshaji wa biashara katika zama hizi za utandawazi umebadilika kutokana na maendeleo makubwa katika nyanja za tekinolojia ya habari na mawasiliano..

Pia ni lazima wote tukubali kuwa sikuhizi biashara ya kutunza kumbukumbu kwenye madaftari ama kukodi fremu mbali ya kuwa inatugharimu pesa nyingi lakini pia imepitwa na wakati.

kwa sababu kuweka kumbukumbu kwemye daftari hakuwezi kukuambia katika muda husika duka ama biashara yako inathamani kiasi gani nikiimaanisha stock in real time. pia kukodi fremu ni gharama kwa sababu inabidi ulipe kiasi kikubwa cha kodi hasa kama unahitaji sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu hivyo basi kutokana na na sababu hizo ndio maana unahitaji kukarabati biashara yako bila kujali ukubwa wake ili uweze kupata faida zaidi.

Unahitaji mfumo wa kukupatia taarifa za biashara yako wakati wowote unapohitaji Real time informationi bila kujali upo katika eneo la biashara ama la.

Unahitaji mfumo wa kutangaza biashara yako bila kutumia nguvu nyingi na pesa, unahitaji nyenzo ya kitekinolojia inatayokugharimu kidogo huku ikikuletea faida kubwa.

Ili uweze kufikia hapo unahitaji kuwasiliana na LenduliTechnologies wataalamu waliobobea katika kutengeneza mifumo imara itakayokuletea ufanisi katika biashara yako

Unaweza kuwasiliana kwa kutumia barua pepe; lenduli@yahoo.com, ama simu ya mkononi: 0717 063294. Kwa ushauri zaidi.  

 

Mtanda wa Google (Google ps) wavamiwa na kubandikwa tangazo

Mtandao wa Google wa Palestina umevamiwa na maharamia wa mtandao na kubandika tangazo lililosomeka “Mjomba google tunakusalimu kutoka Palestina kukukumbusha kuwa jina la nchi kwenye ramani ya google (Google maps) sio Israel bali ni Palestina.” maharamia hao waliendelea kwa kuuliza swali; kwani ni kitu gani kitatokea kama tutafanya mapinduzi na kubadili jina la nchi ya Israel  kuwa Palestina kwenye ramani ya google!” Yatakuwa mapinduzi makubwa hivyo Rihana sikiliza na kuwa mpole”

Habari kutoka google; wamefanikiwa kuliondoa bandiko hilo muda mfupi uliopita.

Usalama kwenye mtandao wa Western Union Mashakani

Kundi la maharamia wa mtandao wa Internet kwa jina la “Cyber Rog” wametoa video inayoonyesha udhaifu katika kubadilisha nuila ama password kwa watumiaji wa mtandao wa Western Union.

Wataalamu wa mambo ya ulinzi na usalama wa mitandao wanasema kwamba video hiyo itaweza kufanikisha maharamia kufanya shambulio la hatari katika akaunti za wateja wa western Union  kwa kubadilisha nuila ya mtu yoyote na kuiba kiasi kikubwa cha fedha kwenye akaunti zao.

Katika mahojiano ya kipekee na EHN, “Cyber Rog” wamedai kuwa baada ya kugundua udhaifu huo waliwaarifu Western Union kwa njia ya barua pepe lakini katika hali ya kushangaza western Union waliamua kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo kimya kimya tena bila hata ya kujibu barua pepe waliyowatumia.

Hivyo “Cyber Rog” wakaamua kuweka video inayoonyesha udhaifu huo katika mtandao wa You tubeWestern Union Password Reset Exploit [Exclusive] ~ eHackingNews:
http://www.ehackingnews.com/2013/09/western-union-password-reset-exploit.html, gonga hapo ujionee mwenyewe.