JE TUNATUMIAJE SIMU JANJA, PAMOJA NA MITANDAO YA KIJAMII?

Jinsi unavyoweza kuhatarisha maisha yako marafiki zako na jamaa zako kwa kutumia mitandao ya kijamii
Mitandao ya kijamii kama facebook, instagram, badoo nk ni mitandao amabayo imejipatia umaarufu mkubwa sana hasa katika nchi za dunia ya tatu kwa siku za hivi karibuni.Umaarufu wa mitandao hii umetokana na tabia ya asili ya umbea ya wakazi wanoishi kwenye dunia ya tatu na kujikuta wakipost vitu ambavyo vimekua vikiwaharibia maisha yao kwa kiasi kikubwa bila wao kufahamu na kupata madhara ya muda mrefu yanayoweza kupelekea matatizo ya kisaikolojia ama hata kifo. Sababu ya pili iliyofanya mitandao hii kuwa maarufu zaidi ni kushuka kwa bei ya simu janja (SMART PHONES) hivyo kupelekea upatikanaji wake kuwa rahisi zaidi na kupelekea watumiaji wengi kuweza kumiliki simu hizo na kujiunga kwenye mitandao hiyo ya kijamii bila kuwa na elimu sahihi juu ya malengo na madhumuni ya kuwepo kwake hivyo kujikuta wakipost vitu ambavyo sio tu vinawafunua wao binafsi bali pia jamaa zao na mataifa yao kwa ujumla na hivyo kupelekea mmomonyoko wa maadili Machafuko, Utekwaji, na udahalilishaji katika taifa. Kwa mfano ni jambo la kawaida siku za hivi karibuni kumkuta mtu amepiga picha ya utupu, ama nusu uchi ama kaburi kwenye hizi nchi za jumuia ya tatu na kuandika status kwenye mtandao wa kijamii guu la bia, kiuno nyigu ama ndo tunazika sasa, ama mtu anampongeza mke wake, mume wake ama motto wake anaekaa nae nyumba moja kwenye mtandao wa kijamii, ama mtu anamtukana jirani yake kwenye mtandao wa kijamii, ama mtu anakula chakula cha jioni halafu anaandika status inatokea sasa hivi (It is happening now) na mambo kadhaa ya kushangaza bila kujua kuwa hayo ni mambo yake binafsi na yalitakiwa kuendelea kuwa binafsi.
Mimi nadhani matumizi bora ya mitandao ya kijamii ni kama kutangaza biashara ama ujuzi wako ili uweze kufahamika na labda ikuletee tija.
Ushauri wangu ni kuwa jamii yetu pamoja na utamaduni wetu wakutopenda kufanya kazi na kujikita zaidi kwenye mambo ya umbea ni lazima tutambue kuwa unapoweka kitu kwenye mtandao inamaana umekiweka ili kila mtumiaji akione hata kama ni chako binafsi wazungu wanasema (Once online it is there to stay) ina maana mtoto wako ambaye hata bado hajazaliwa siku akikua hata kama wewe umefariki anaweza kuona vitu vya hovyo ulivyokua unaposti. Mimi nikiamua kuwa mwizi na kwakutumia taaluma yangu ya kuzifahamu tekinolojia mbalimbali za mawasiliano ninaweza kukuibia kutokana na information zako unazoziweka mtandaoni kwa kutumia ukandarasi wa kijamii ama (Social engineering), mtekaji anaweza kukuteka, Majasusi na watu wenye husda ni rahisi kuifanyie nchi yetu ujasusi kwa kutumia taarifa tunazopost kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia teknolojia ya (big data mining) na kizifanya nchi zetu zisiendelee kiuchumi kwa sababu ni rahisi kukusanya taarifa za uelewa wa watu wan chi fulani kwa kuanza kukusanya taarifa zao kwenye mitandao ya kijamii ka facebook, instagram, watsapp, badoo n.k
Pia ningependekeza serikali iongeze maradufu kodi za simu janja (smart phones) ili zisiwafikie watu wengi zaidi na kuleta matatizo kama hayo niliyoyataja hapo juu.